IQNA

AI yalaani kutiwa nguvuni Waislamu nchini Nigeria

17:12 - August 31, 2018
Habari ID: 3471654
TEHRAN (IQNA)-Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limelaani hatua ya serikali ya Abuja ya kuwaweka kizuizini kinyume sheria Waislamu hasa wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Amnesty International ilitoa taarifa hiyo jana na mbali na kulalamikia kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria wananchi wa Nigeria kwa tuhuma zisizo na uthibitisho kama madai ya kujihusisha na vitendo vya kigaidi au kuwa wafuasi wa mrengo unaotaka kujitenga eneo la Biafra imesema kuwa, katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, maelfu ya wananchi wametiwa mbaroni kwa madai hayo na pia kwa madai ya kuwa wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Amnesty International, wanachama 600 wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria hawajulikani walipo hadi hivi sasa na kwa miaka kadhaa sasa familia nyingi zimekuwa zikitafuta jamaa zao bila ya mafanikio.

Itakumbukwa kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky akiwa na mke wake walitekwa nyara na Jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 wakati askari walipovamia kituo chake cha kidini huko katika mji wa Zaria jimboni Kaduna. Tokea wakati huo Sheikh Zakzaky na mkewe wamekuwa wakizuiliwa katika mojawapo ya vituo vya kijeshi vya nchi hiyo bila kufunguliwa mashtaka.

Uvamizi huo ulijiri baada ya Jeshi la Nigeria kudai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria walikuwa na njama ya kutaka kumuua mkuu wa jeshi hilo, madai ambayo yalikanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo.Inakadiriwa kuwa Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa katika tukio hilo.

3466654

captcha