IQNA

Siku ya Kimataifa ya Quds, Mombasa, Kenya

9:53 - June 01, 2019
Habari ID: 3471979
TEHRAN (IQNA)- Wakaazi wa mji wa Mombasa nchini Kenya wamejumuika na Waislamu na wapenda haki kote duniani katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, kwa lengo la kuunga mkono ukombozi wa Palestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Miaka 41 iliyopita yaani katika Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani ya mwaka 1399 Hijria, Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitoa ujumbe muhimu sana na kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds. Imam Khomeini aliita siku hiyo kuwa ni ya kuipa uhai mpya dini tukufu ya Kiislamu. Kuanzia mwaka huo hadi leo hii, Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani ya kila mwaka huadhimishwa nchini Iran na katika maeneo mengine mengi duniani kwa maandamano makubwa ya Waislamu ya kulaani jinai za wavamizi wa Quds na kutangaza uungaji mkono wao kwa malengo matukufu ya wananchi wa Palestina. Kila mwaka maandamano na maadhimisho hayo hufanyika kwa kufana zaidi kuliko mwaka uliopita. Siku ya Kimataifa ya Quds imepata uungaji mkono mkubwa wa Waislamu kote ulimwenguni na kuthibitisha kuwa kadhia ya Quds na Palestina haiwezi kuamuliwa kwenye vikao vya faragha vya baadhi ya watu kwani Waislamu hivi sasa wameamka kutokana na dhulma kubwa wanayofanyiwa Wapalestina na wameamua kusimama kidete kupambana na utawala dhalimu wa Israel. Katika ujumbe wake huo wa kuanzisha Siku ya Kimataifa ya Quds, Imam Khomeini MA alisema: “Ninawaomba Waislamu na tawala zote za nchi za Waislamu waungane katika mapambano ya kukata mikono ya dhalimu huyu (Israel) na wasaidizi wake na ninawaomba Waislamu wote duniani kuihesabu Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa Quds ili kuonesha uungaji mkono wa kimataifa wa Waislamu katika kulinda haki za kisheria za wananchi Waislamu wa Palestina.”

Siku ya Kimataifa ya Quds, Mombasa, Kenya

Siku ya Kimataifa ya Quds, Mombasa, Kenya

Siku ya Kimataifa ya Quds, Mombasa, Kenya

Siku ya Kimataifa ya Quds, Mombasa, Kenya

Siku ya Kimataifa ya Quds, Mombasa, Kenya

 

 

captcha