IQNA

Mahfali ya Qur'ani ya al Kauthar yafanyika Qatif

14:12 - September 04, 2010
Habari ID: 1986938
Mahfali ya Qur'ani ya al Kauthar ilifanyika jana usiku katika msikiti wa al Zahra (as) katika mji wa Umm al Hammam katika mkoa wa Qatif nchini Saud Arabia.
Mahfali hiyo ya kisomo cha Qur'ani ilihuhduriwa na makari wa eneo hilo lenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia.
Mahfali hiyo ilianza saa nne usiku kwa kisomo cha Qur'ani kilichowashirikisha pia wasomaji mashuhuri wa eneo la mashariki mwa Saudia.
Wakati huo huo miji ya Qatif, Ihsa, al Khubar, Dammam na miji mingine yenye idadi kubwa ya Waislamu wa madehebu ya Shia nchini Saudi Arabia mwaka huu imeshuhudia harakati kubwa za maombolezo ya kuuawa shahidi Imam wa kwanza katika kizazi cha Bwana wetu Muhammad (saw) Imam Ali bin Abi Twalib (sa). Shughuli hizo zimehudhuriwa na idadi kubwa ya waombolezaji na wapenzi wa Ahlulbait (as).
Shughuli za maombolezo ya kukumbuka siku ya kuuawa shahidi Imam Ali bin Abi Twalib (as) za mwaka huu zimefana mno licha ya kushadidi ukandamizaji wa kimadhehebu dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na mashinikizo dhidi yao nchini Saudi Arabia.
Waislamu wa madhehebu ya Shia wanakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 15 ya jamii ya Saudi Arabia. 647006


captcha