IQNA

Masomo ya hifdhi na tajweedi ya Qur'ani kwa wanafunzi wa shule za msingi yaanza Qatif, Saudi Arabia

10:11 - October 21, 2010
Habari ID: 2016929
Masomo ya hifdhi na tajweedi ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa wanafunzi wa shule za msingi chini ya anwani 'Sote tuelekee kwenye jamii ya Qur'ani' yalianza siku ya Jumanne tarehe 19 Oktoba huko katika mkoa wa Qatif nchini Saudi Arabia
Masomo hayo ambayo yanadhaminiwa na Kituo cha Qur'ani Tukufu cha Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya mji wa Safawi katika mkoa wa Qatif yatakuwa yakifanyika katika misikiti ya al-Kauthar, Rasul al-A'dham (saw) na Imam Ridha (as).
Masomo hayo ambayo yatakuwa yakifanyika mara nne kwa wiki yataendelea kwa muda wa miezi mitatu. Licha ya kuhifadhi juzuu tofauti za Qur'ani, wanafunzi pia watafundishwa masomo mbalimbali yanayofungamana na tajweedi na shakhsia wa Qur'ani.
Masomo hayo yamelenga kuwalea wanafunzi kwa msingi wa thamani na maadili ya Kiislamu. Wasimamizi wa masomo hayo wamesema kuwa masomo mengine ya kiutamaduni, kielimu na kijamii yatatolewa na walimu mashuhuri pambizoni mwa masomo hayo ya Qur'ani. 679250
captcha