Kituo cha upashaji habari cha al Kauthar kimeripoti kuwa Waziri wa Utamaduni wa serikari halali ya Palestina Usama al Isawi amesema kuwa zaidi ya filamu 70 zimewasilishwa katika tamasha hilo.
Amesema kuwa ujumbe wa nchi zinazoshiriki katika tamasha hilo ni mshikamano na wananchi wa Palestina na kwamba kuna matumaini kwamba mfungamano huo utaendelezwa katika siku zijazo.
Katika upande mwingine Mustafa Hijazi ambaye ni mwanaharakati wa vyombo vya habari wa Palestina amesema kuwa filamu za tamasha hilo zinasimulia na kufichua jinai zinazofanywa na Wazayuni wa Israel dhidi ya raia wasiokuwa na hatia wa Gaza.
Sherehe za ufunguzi wa tamasha hilo zimehudhuriwa na wasanii na wanahabari wa Palestina na nchi za Kiarabu. 709354