IQNA

Kongamano la Kimataifa la Mashia Misri

12:53 - December 26, 2010
Habari ID: 2053097
Kongamano la Kwanza la Kimataifa ambalo limeitishwa na Mashia wa Misri linatazamiwa kufanyika mjini Cairo na kuhudhuriwa na wasomi wa ulimwengu wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa tovuti la Al Kauthar, Muhammad al Darini Mkuu wa Baraza Kuu la Ahul Bayt AS nchini Misri, kongamano hilo litafanyika kwa lengo la kukabiliana na ugaidi na kusisitiza kuhusu umoja na mashikamano wa Waislamu. Ameongeza kuwa shakhsia na wasomi kutoka nchi za Kiislamu watahudhuria kongamano hilo.
Ameongeza kuwa kati ya watakaohudhuria kongamano hilo ni Saleh Al Heidary Mkuu wa Baraza la Waqfu wa Kishia la Iraq, Ahmad As-Samarai Mkuu wa Baraza la Waqfu wa Masuni Iraq, Sayyid Muqtada Sadr Kiongozi wa Harakati ya Sadr ya Iraq na Ahmad Sayyed Safi mwakilishi wa Ayatullahil Udhma Ali Sistani.
Mkuu wa Baraza Kuu la Ahul Bayt AS nchini Misri amesema barua za mwaliko zimetumwa baada ya Chuo Kikuu cha Al Azhar kuafiki suala hili. Amongeza kuwa shakhsia wa Misri wanaotazamiwa kuhudhuria kongamano hilo ni Mufti wa Misri Sheikh Ali Gomaa na Mkuu wa Jumuiya ya Waandishi Habari Misri Makzam Muhammad Ahmad kati ya wengine.
Imearifiwa kuwa Baraza Kuu la Ahul Bayt AS nchini Misri pia limeshamwalika Sheikh Mkuu wa Al Azhar Ahmad Tayyib kushiriki katika kongamano hilo la kimataifa la kupambana na ugaidi.
717973

captcha