IQNA

Fatuwa ya Ayatullah Khamenei tukio muhimu zaidi la kidini katika mwaka 2010

16:28 - December 26, 2010
Habari ID: 2053628
Fatuwa iliyotolewa na Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran akiharamisha kuwavunjiwa heshima shakhsia wanaoheshimiwa na Waislamu wa madhehebu ya Suni imetajwa kati ya matukio 10 muhimu zaidi ya kidini katika mwaka huu unaomalizika wa 2010.
Kanali ya televisheni ya al Kauthar imeripoti kuwa hatua ya Sheikh Yasir al Habib mwanazuoni wa Kishia wa Kuwait ya kumvunjia heshima Bibi Aisha mke wa Mtukufu Mtume Muhammad (saw) iliakisiwa kwa kiwango kikubwa katika duru za Kishia na Kisuni na kwa sababu hiyo Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alitoa fatuwa akiharamisha kuvunjiwa heshima Bibi Aisha na shakhsia wengine wanaoheshimiwa na Waislamu wa madhehebu ya Suni. Fatuwa hiyo ilikaribishwa mno na Waislamu wa Kisuni na Kishia.
Kituo cha habari cha On Islam ambacho kimetegemea tathmini ya wataalamu na ripoti za vyombo vya habari vya nchi za Magharibi na za Kiarabu likiwemo jarida la Times la Marekani, kimesema kuwa fatuwa ya Ayatullah Ali Khamenei ya kuharamisha kuvunjiwa heshima matukufu ya Wasuni ni miongoni mwa matukio 10 muhimu zaidi ya kidini katika mwaka huu wa 2010.
Wataalamu wanasema kuwa fatuwa hiyo ilitolewa katika kipindi nyeti na ilizua kutokea vita vya kimadhehebu kati ya Shia na Suni katika nchi mbalimbali za Kiislamu hususan katika eneo la Mashariki ya Kati.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Sheikh Yasir al Habib wa Kuwait mwezi Ramadhani uliopita aliwakasirisha mno wafuasi wa madhehebu ya Kisuni mjini London kwa kuitisha marasimu ya kuadhimisha siku ya kufariki dunia Bibi Aisha, mke wa Mtume Muhammad (saw).
Kituo cha On Islam kimetaja wito wa Kasisi Terry Jones wa Florida nchini Marekani wa kufanyika siku ya kimataifa ya kuchomwa moto Qur'ani Tukufu katika kumbukumbu ya Septemba 11, mradi wa ujenzi wa msikiti karibu na eneo la majengo mapacha mjini New York Marekani, kushadidi chuki na uhasama dhidi ya Uislamu barani Ulaya, kuchaguliwa Ahmad al Tayyib kuwa Sheikh mpya wa al Azhar na matamshi ya kasisi wa Misri ya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu kuwa mi miongoni mwa matukio muhumu zaidi ya kidini katika mwaka huu wa 2010. 718440


captcha