IQNA

Mashia wa Uingereza kuomboleza Arbaini ya Imam Hussein (as)

13:42 - January 19, 2011
Habari ID: 2067285
Huku Arbaini ya Imam Hussein (as), mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) ikizidi kukaribia, wafuasi wa madhehebu ya Ahlul Bait (as) nchini Uingereza wanajiandaa kushiriki vilivyo katika maombolezo hayo yaliyopangwa kufanyika siku ya Jumapili Januari 23.
Kwa mujibu wa tovuti ya al-Kauthar, Mashia na wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) wamepanga kufanya maandamano ya maombolezo siku ya Jumapili ili kuonyesha mfungamano wao na mamilioni ya waomboleza wa Imam Hussein (as) ambao wanatembea kwa miguu kutoka kila pembe ya Iraq ili kushiriki kwenye maombolezo ya Arbaini katika mji mtakatifu wa Karbala. Maombolezo hayo ambayo yatawashirikisha watu wa jamii mbalimbali wanaoishi nchini Uingereza yatafanyika katikati ya mji wa London.
Kila mwaka Waislamu wa Uingereza hufanya maombolezo ya Arbaini ya Bwana wa Mashahidi Imam Hussein (as) katika siku ya mapumziko inayokaribiana zaidi na siku hiyo ya majonzi makubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Maombolezo ya mara hii ya Imam Hussein yamepangwa kufanyika siku ya Jumapili kwa kutilia maanani kwamba ndiyo siku iliyo karibu zaidi na siku hiyo ya maombolezo. 732994
captcha