Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Al Kauthar, hafla hiyo ya maombolezo imeandaliwa na msimamizi wa Haram ya Imam Hussein AS.
Al Haj Qasim Al Avad mkuu wa makundi ya kidini Karbala amesema huu ni mwaka wan ne mfululizo ambapo mji wa Karbala umeteuliwa kuwa mwenyeji wa hafla hizo za siku kumi nchini Iraq.
Bibi Fatima Zahra SA anachukuliwa na Waislamu kuwa kigezo cha kuigwa hasa na wanawake. Bibi Fatima daima alikuwa na Mtume SAW wakati alipokuwa akikabiliwa na masaibu mikononi mwa kabila la Qureishi mjini Makka. Baada ya kuhamia Madina, Bibi aliolewa na Imam Ali AS, binamu yake Mtume SAW na walijaaliwa watoto wanne. Bibi Fatima aliuawa shahidi miezi kadhaa baada ya kuaga dunia Mtume SAW na alizikwa katika eneo la Jannat al Baqi mjini Madina. Eneo haswa la kaburi lake halijulikani.
772274