IQNA

Kikao cha tatu cha Mawaziri wa Afya wa nchi za Kiislamu chafanyika

16:46 - October 01, 2011
Habari ID: 2196696
Kikao cha tatu cha Mawaziri wa Afya wa Nchi za Kiislamu kilianza siku ya Alkhamisi huko katika mji wa Astana ambao ni mji mkuu wa Kazakhstan.
Kikao hicho kilifunguliwa kwa hotuba ya Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC. Katika hotuba hiyo, Ihsanoghu aliwataka Mwaziri wa Afya wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kutilia maanani suala la afya na tiba pamoja na kutathmini hali nzima ya afya inayotawala katika nchi za Kiislamu.
Mbali na mawaziri hao wa nchi za Kiislamu wawakilishi wa mashirika kadhaa ya kimataifa yanayoshughulikia kwa njia moja au nyingine masuala ya afya duniani yakiwemo ya WHO, UNESCO, shirika la kupambana na maradhi ya polio na mfuko wa kimataifa wa kupambana na maradhi ya UKIMWI wameshiriki pia katika kikao hicho.
Namna ya kufikiwa malengo ya maendeleo ya milenia ya tatu, kupunguza vifo vya watoto, kuimarisha hali ya afya ya akina mama na njia za kupambana na maradhi kama vile ya kupooza au polio, Ukimwi, surua na Malaria ni miongoni mwa masuala ambayo yamejadiliwa katika kikao hicho. 870128
captcha