Taarifa iliyotolewa na OIC imesema kuwa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiislamu watakutana tarehe 26 Novemba kwa shabaha ya kujadili na kuchunguza matukio ya Syria.
Mkutano huo utawahamasisha wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya OIC kukutana na kufanya mazungumzo na serikali ya Syria na wapinzani wake. Kamati hiyo inajumuisha nchi za Djibouti, Malaysia, Saudi Arabia, Misri, Senegal, Kazakhstan, na Tajikistan.
Kikao hicho kinafanyika baada ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Ekmeleddin Ihsanoglu kutahadharisha juu ya njama zinazofanywa za kutaka kuufanya mgogoro wa Syria kuwa wa kimataifa. Amesisitiza kuwa nchi za Kiislamu zinapinga uingiliaji wowote wa kigeni katika masuala ya Syria. 901583