IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tatarstan

16:34 - November 26, 2011
Habari ID: 2228499
Mashindano ya Nane ya Kimataifa ya Qur’ani yameanza katika mji wa Kazan, Jamhuri ya Tatarstan.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maqari na mahufadh 35 wa Qur’ani kutoka Russia, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Ukraine, Belarus, Azerbaijan, Uzbekistan na Tajikistan wanashiriki katika mashindano hayo yaliyoanza Novemba 24.
Mashindano hayo yameandaliwa na Kituo cha Kutoa Mafunzo kwa Maqari wa Qur’ani katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Russia.
Sherehe ya ufunguzi wa mashindano hayo ilihudhuriwa na Sheikh Musa Mirza Mkuu wa Waqfu wa Ihsan wa Kyrgyzstan na wanazuoni wengine wa ngazi za juu wa Tatarstan.
Jamhuri ya Tatarstan ambayo mji wake mkuu ni Kazan ni sehemu ya Shirikisho la Russia na iko katika Jimbo la Volga.
902555
captcha