IQNA

Iran kuanzisha kanali ya TV ya Kihispania

10:12 - December 18, 2011
Habari ID: 2240338
Shirika la Utangazaji la Iran -IRIB- litaanzisha kanali ya televiesheni ya lugha ya Kihispania itakayo rusha hewani vipindi mbalimbali kwa wanaozungumza lugha hiyo kote duniani.
Kanali hiyo ijulikanayo kwa jina la Hispan TV itazinduliwa siku ya Jumatano na inakusudia kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni kati ya Iran na nchi zinazozungumza Kihispania duniani.
Hispan TV ambayo makao yake yatakuwa mjini Tehran ina maripota kote duniani na itaanza kurusha matangazo kwa masaa 16 na hatimaye masaa 24. Hispan TV ina tovuti ya intaneti yenye anwani ya www.hispantv.com na www.hispantv.ir. Mbali na kwenye satalaiti, matangazo ya Hispan TV yanarushwa moja kwa moja kupitia tovuti hizo.
Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tayari kina kanali za televisheni za lugha ya Kiarabu kama vile Al Alam, Al Kauthar na IFILM. Aidha kuna kanali ya lugha ya Kiingereza, Press TV mbali na kanali ya Sahar ambayo inatangaza kwa lugha za Kifaransa, Kiingereza, Kiurdu, Kibosnia, Kikurdi na Kiazari.
917303
captcha