IQNA

Iran kuandaa kongamano la wanawake Waislamu wanahabari

15:59 - January 02, 2012
Habari ID: 2249696
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapanga kuandaa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Waandishi Habari wanawake ili kuwatia motisha wanawake Waislamu na kustawisha maadili ya Kiislamu.
Zaidi ya wawakilishi wa magazeti na majarida 27 kutoka mabara ya Asia, Afrika , Amerika na Ulaya wametangaza nia ya kushiriki katika kongamano hilo. Waandisha habari wanawake kutoka Iran pia watashiriki na wenzao wa kigeni. Kati ya nchi zilizotangaza kushiriki ni pamoja na Iraq, Tunisia, Misri, Russia , Bosnia na Herzegovina, Kosovo, Kazakhstan, Argentina na Thailand.
Kati ya malengo ya kongamano hilo ni kuarifisha majarida na magazeti ya wanawake Waislamu kutoka maeneo yote ya dunia. Aidha waandalizi wa kongamano hilo wana matumaini kuwa washiriki wataweza kuimarisha uwezo na ushirikiano wao ili kuinua kiwango cha vyombo vya habari vya Kiislamu. Kongamano hilo litaanza tarehe 7 mwezi huu wa Januari katika mji mkuu wa Iran, Tehran na kuendelea kwa siku saba.
926662
captcha