IQNA

Mwanachama wa Harakati ya Kuteka Wall Street asilimu

11:59 - February 07, 2012
Habari ID: 2269979
Mmoja kati ya wanachama wa Harakati ya Kuteka Wall Street inayopinga ubepari na dhulma nchini Marekani ametangaza kusilimu na kukubali dini tukufu ya Kiislamu katika kipindi cha moja kwa moja cha Kanali ya Kimataifa ya Televisheni ya Al Kauthar.
Kwa mujibu wa idara ya habari ya Televisheni ya Al Kauthar yenye makao yake Iran, Monica Waite ambaye alikuwa akihojiwa katika kipindi cha 'Kadhia Sakhinat' amesema: 'Baada ya kuona ukweli kuhusu Iran na Uislamu, nimefahamu namna vyombo vya habari vya Kimagharibi vinavyopotosha ukweli kuhusu Iran na Uislamu. Kwa hivyo nimesimama kidete mbele ya njama hizi na kuanzia sasa natangaza kuikumbatia dini tukufu ya Kiislamu na nitatumia uwezo wango wote kujifunza kikamilifu kuhusu Uislamu'.
Akiendelea na mahojiano hayo ameashiria kuhusu hali ya kisiasa na kijamii Marekani na kusema: 'Kile ambacho kinaendelea Marekani leo ni tone katika bahari. Siku za usoni kutajiri matukio makubwa zaidi. Wamarekani wamechoshwa na sera za serikali za kibeberu na kujitanua na kutoridhika huku kunatangazwa kwa njia mbalimbali'.
Kanali ya televisheni ya Al Kauthar inayotangaza kwa lugha ya Kiarabu hivi karibuni ilianza kurusha matangazo yake Marekani na Canada. Kanali ya Al Kauthar ilianza kurusha matangazo yake mwaka 2002 katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika na sasa inapatikana katika maeneo yote duniani.
948802
captcha