Sherehe hizo ambazo ziliandaliwa na Shule ya Kiislamu ya Mashia wa Sao Paulo zilifanyika hapo jana Jumatatu. Wafanyakazi na wanafunzi wa kike na kiume wa shule hiyo walioandamana na wazazi wao walishiriki kwa wingi katika sherehe hizo, ambapo Bibi Hayat mshauri wa masuala ya kidini wa shule hiyo aliwahutubia hadhirina kuhusiana na maisha na fadhila za kimaadili za Bibi Fatma (as). Wanafunzi walifanya michezo ya kuigiza na kuimba kasida za kumsifu Bibi Fatma (as) pamoja na nafasi ya mama katika jamii. Wanafunzi wa shule iliyotajwa pia waliwapa zawadi wazazi kazi za sanaa walizokuwa wamezitayarisha kwa mikono yao wenyewe katika shule hiyo. 1008540