Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, ukumbi huo umefunguliwa katika hafla iliyomshirikisha Sheikh Al Bukai, Imamu wa Msikiti wa Pari mjini humo pamoja na Waislamu wa eneo hilo.
Sheikh Hassan Borji ,Imamu wa Msikiti wa Mohammad Rasulullah SAW katika mji wa Sao Paulo atakuwa katika ukumbi kuwa mara mbili kwa wiki kwa lengo la kusalisha sala ya Jamaa.
Ukumbi huo wa sala umefadhiliwa na Waislamu wenye asili ya Lebanon waishio nchini Brazil na moja ya malengo yake ni kuimarisha umoja wa Waislamu nchini humo na pia kuandaa mazingira ya Waislamu kujuana.
Sao Paulo ni mji mkubwa wenye idadi ya watu takribani milioni 30.
1015945