Hicho ni kikao cha kwanza kufanyika katika mfululizo wa vikao kama hivyo vinavyotazamiwa kufanyika hivi karibuni kati ya dini ya Kiislamu na Wakristo kwa lengo la kukurubisha pamoja fikra za wafuasi wa dini mbili hizi, kuhusiana na masuala muhimu ya kimataifa na kidini. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi mkuu wa taasisi iliyotajwa mjini Tehran. Wanafikra na wasomi wengi wa Kiislamu na Kikristo kutoka nchi za Iran, Lebanon, Syria, Uswisi, Denmark, Brazil, Pakistan, Armenia na Uingereza wameshiriki katika kikao hicho muhimu. 1017461