IQNA

Televisheni ya al-Kauthar yatangaza moja kwa moja usomaji wa Qur'ani katika Haram ya Imam Ali (as)

13:27 - August 07, 2012
Habari ID: 2387624
Televisheni ya maarifa ya Ahlul Bait wa Mtume (saw) imekuwa ikirusha hewani vipindi tofauti vya usomaji na hifdhi ya Qur'ani Tukufu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Akibainisha suala hilo Hujjatul Islam wal Muslimin Abdallah Ridhai, mkuu wa kitengo cha utamaduni na maarifa ya Kiislamu cha televisheni hiyo amesema maarifa sahihi ya Kiislamu na hasa ya Qur'ani Tukufu yana nafasi muhimu katika televisheni hiyo hususan katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ambao ni mwezi wa kuteremshwa kitabu hicho cha mbinguni kwa Mtume Mtukufu (saw) kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu.
Ameendelea kusema kuwa vipindi maalumu vya usomaji Qur'ani vimekuwa vikirushwa hewani moja kwa moja katika haramu tukufu za Imam Ali (as) mjini Najaf Iraq, Imam Ali Ridha (as) mjini Mash'had na Bibi Fatima Maasuma (as) mjini Qum Iran katika mwezi huu mtukufu jambo ambalo limewavutia watazamaji wengi wa televisheni hiyo.
Ridhai amesema vipindi vingine ambavyo vimewavutia watazamaji ni vile vinavyozungumzia maisha ya makarii na mahafidh wa Qur'ani Tukufu, maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran na vilevile habari zinazohusiana na Qur'ani kutoka pambe tofauti za dunia. 1072504
captcha