IQNA

Mchezaji soka Ligi ya Bundesliga ya Ujerumani asilimu

16:08 - January 29, 2015
Habari ID: 2779913
Mchezaji soka nchini Ujerumani Danny Blum ametangaza kusilimu na kuutaja Uislamu kuwa dini ya matumaini na nguvu.

'Uislamu nanipatia matumaini na nguvu. Sala inautuliza moyo wangu," Blum ameliambia gazeti la Bild, Jumatatu, Januari 26.
Ameongeza kuwa, "zamani nilikuwa mtu mwenye kupandwa hasira haraka na sikuwa na utambulisho maalumu maishani." Blum aljiunga na timu ya soka ya 1. FC Nürnberg ya Bavaria mwezi Julai mwaka 2014. Timu hiyo iko katika Divisheni ya Pili ya mpira wa kulipwa katika Ligi ya Ujerumani, Bundesliga. Baada ya kujiunga na timu hiyo aliumiza goti lake na kulazimika kuchukua likizo ya miezi sita.
Mapema mwezi huu wa Januari 2015 aliamua kuikumbatia dini tukufu ya Kiislamu maishani. Uislamu ni dini inayostawi kwa kasi zaidi duniani. Anasema pamoja na kuwa hakuwa na matatizo ya kifedha maishani alitafakari sana kuhusu mustakabali wake.
"Niliutembelea msikiti na punde baada ya hapo moyo wangu uliweza kuhisi mabadiliko. Nilihisi kuwa nataka kujua mengi," ameliambia gazeti la Bild. Baada ya kusilimu, Blum anasema yeye huswali Sala tano kila siku na hula chakula halali. Mchezaji soka huyu mwenye umri wa miaka 24 anasema wazazi wake walishangaa sana alipowafahamisha uamuzi wake kwa mara ya kwanza. "Ni Wakristo wenye kufungamana na Ukristo. Lakini baadaye walikubali uamuzi wangu maadamu naamini ndio njia sahihi," amesema.
Mjerumani huyu aliyeseilimu anasema: "Uislamu ni dini ya amani. Imani yangu kamwe haimlazimu mtu kufanya asichokitaka.  Nimesilimu kwa hiari yangu." Nchini Ujerumani kuna Waislamu karibu milioni 4 huku 220,000 wakiwa wanaishi katika mji mkuu Berlin. Watu wenye asili ya Uturuki ni karibu thuluthi mbili ya Waislamu wote Ujerumani.../mh

2768964

captcha