IQNA

Kampeni ya kimataifa ya kutaka kuachiliwa huru Ayatollah Nimr

15:02 - August 04, 2015
Habari ID: 3338914
Kampeni ya kimataifa imeanzishwa kwa lengo la kuushinikikza utawala wa Saudi Arabia kumuachilia huru msomi wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia Sheikh Nimr al-Nimr.

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya Al-Alam, maandamano yamefanyika katika nchi mbali mbali duniani kuanzia Ijumaa kulaani hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama ya Saudia dhidi ya Sheikh Nimr.
Maandamano yamefanyika katika miji kama vile Sydney, Australia, Auckland, New Zealand, Mexico City nchini Mexico, Sao Paulo, Brazil, Brussels, Belgium, na Paris, Ufaransa.

Sheikh Nimr alitiwa mbaroni mwezi Julai mwaka 2012 kufuatia maandamano ya wananchi katika eneo la Qatif nchini Saudi Arabia.
Anatuhumiwa kuwa alitoa hotuba zilizo dhidi ya utawala wa kifalme na kuwatetea wafungwa wa kisiasa. Kukamatwa Sheikh Nimr kuliibua machafuko makubwa katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Mwezi Machi mwaka huu mahakama ya rufaa ya Saudia iliidhinisha hukumu ya kifo dhidi ya mwanazuoni huyo wa Kiislamu lakini hukumu hiyo ya kidhalimu bado haijatekelezwa.../mh

3338672

captcha