IQNA

Jeshi la Nigeria labomoa kaburi la mama wa Sheikh Zakzaky

6:18 - December 25, 2015
Habari ID: 3469062
Jeshi la Nigeria limeendelea na hujuma zake dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia baada ya kubomoa Huseiniyyah nyingine katika mji wa Zaria ulioko katika jimbo la Kaduna.

Hicho ni kituo cha pili cha kidini cha Waislamu wa madhehebu ya Shia kubomolewa na jeshi la Nigeria katika mji wa Zaria katika kipindi cha chini ya juma moja. Jumatatu ya wiki hii pia, jeshi la Nigeria liliibomoa kikamilifu Huseiniyyah ya Baqiyyatullah katika mji wa Zaria ambao ni makao makuu ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Wakati huo huo ripoti kutoka Nigeria zinasema kuwa, leo pia jeshi la nchi hiyo limebomoa kaburi la mama yake Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Jeshi la Nigeria likiwa na buldoza lilifika katika kaburi la marehemu Hajja Saleha Muhammad, mama wa Sheikh Ibrahim Zakzaky lililoko kaskazini mwa mji wa Zaria na kulibomo kikamilifu.

Hayo yanajiri katika hali ambayo siku chache zilizopita, jeshi la Nigeria liliishambulia Husainiyyah ya Baqiyyatullah katika mji wa Zaria pamoja na nyumba ya Sheikh Ibrahim Zakzaky na kuwaua mamia ya Waislamu kwa kisingizio kwamba Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilikula njama ya kutaka kumuua mkuu wa jeshi na kufunga njia kwa ajili ya shughuli za mijumuiko ya kidini ya harakati hiyo.

3468977

captcha