IQNA

Bidhaa Halali zazidi kuwavutia wengi duniani

10:10 - February 04, 2016
Habari ID: 3470113
Kumetabiriwa ongezeko la utumizi wa vyakula, bidhaa na huduma halali duniani kwa asilimia 10.8 hadi mwka 2019 na hivyo kuibua biashara yenye thamani ya dola trilioni 3.7.

Kwa mujibu wa ripoti ya Uchumi wa Kiislamu Duniani iliyofadhiliwa na serikali mji wa Dubai na kutayarishwa na mashirika ya ThomsonReuters na DinarStandard, mwaka uliopita wa 2015 umeshuhudia ustawi mkubwa katika soko la vyakula na mtindo wa maisha halali. Kati ya hatua zilizopigwa ni shirika kubwa la vyakula halali Brazil kuwekeza katika kiwanda kipya Imarati pamoja na teknolojia mpya kutoka Ufaransa, Malaysia, na Imarati ambazo zina uwezo wa kukagua vyakula halali.

Halikadhalika kumesuhudiwa kuimarika sekta ya utalii halali unaojumuisha, vyakula, vinywaji na mahoteli hasa katika nchi kama vile Imarati, Maldives, Uhispania, Japan, Ufilipino na Russia.

Hivi sasa utalii halali unashikilia asilimia 11.6 ya utalii wa kimataifa na sekta hiyo inatazamiwa kupata pato la dola bilioni 238 ifikapo mwaka 2019.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, sekta ya vyakula halali pekee itafika trilioni 2.537 ifikapo mwaka 2019 kutoka bilioni 795 mwaka 2014. Nchi za Kiislamu zenye sekta kubwa ya vyakula halali ni pamoja na Uturuki, Pakistan, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Indonesia.

3458973


captcha