IQNA

Qarii Mtanzania ashinda kitengo cha 'Saut na Lahn' Mashindano ya Qur'ani Iran

15:23 - May 18, 2016
Habari ID: 3470317
Majaji katika Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran wametangaza kuwa qarii mshiriki kutoka Tanzania amepata nafasi bora zaidi kwa mtazamo wa 'Saut na Lahn' katika usomaji wake wa Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika sherehe za Jumanne Usiku za kuwaenzi washindi wa Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yaliyofanyika hapa Tehran, baada ya washindi katika vitengo vya hifdh na qiraa kupata zawadi, qarii wa Tanzania Ustadh Rajayi Ayoub amenziwa kutokana na kuwa na sauti na lahni bora zaidi miongoni mwa washiriki wote kutoka zaidi ya nchi 70 duniani.

Uchunguzi wa maoni uliofanywa na IQNA miongoni mwa washiriki kutoka nchi zingine walisema qarii Mtanzania alikuwa na sauti bora zaidi.

Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalizinduliwa rasmi Jumatano iliyopita na kumalizika jana Jumanne katika Ukumbi Mkubwa wa Sala wa Imam Khomeini MA mjini Tehran.

Nchi zaidi ya 70 zilituma wawakilishi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ambayo yalikuwa na washiriki 130. Kaulimbiu ya mashindano ya mwaka huu ilikuwa ni "Kitabu Kimoja Umma Moja”.

Sikiliza/Tizama Qiraa ya Ustadh Ayoub hapo chini

 

3499137

 

 

 

DOWNLOAD

 

captcha