Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo Jumatatu mjini Tehran alipohutubia hadhara ya maelfu ya wananchi kutoka mikoa
mbalimbali ya Iran na kuongeza kuwa ukiukaji wa ahadi wa Washington ni nuta inayothibitisha tena udharura wa
kutokuwa na imani na Wamarekani.
Ayatullah Khameni amesema kuwa mapatano ya JCPOA yameonesha kuwa, njia
ya kupata maendeleo ya nchi na kuboresha maisha ya wananchi,
ni kuzingatia mambo ya ndani na si kuelekea kwa maadui ambao daima
wamekuwa wakitatiza na kuikwaza Iran kieneo na kimataifa. Suala la
kutokuwa na imani na Marekani si nara ya kipropagnda bali ni suala
linalotokana na tajiriba na uzoefu wa huko nyumba, mwenendo wa sasa wa
Marekani na unyambuzi wa kina kuhusu malengo ya kibeberu na kijuba ya
Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.
Masuala hayo matatu yanaweza kutegemewa katika kuchambua matukio ambayo
Marekani ilihusika au kuwa na mchango katika kutokea kwake. Vilevile
ameshiria hali ya Mashariki ya Kati na kusema: Kufichuka wazi uhusiano
wa serikali ya Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel ni hanjari
na jambia katika mgongo wa Umma wa Kiislamu na usaliti mkubwa, lakini
inatupasa kuelelewa kuwa Wamarekani pia wana nafasi katika kosa hilo
kubwa kwa sababu serikali ya Saudia inafuata Marekani.
Katika hotuba hiyo Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia ameashiria
nafasi na mchango wa Marekani katika kuanzisha na kuimarisha makundi ya
kitakfiri kwa shabaha ya kuzusha hitilafu katika Umma wa Kiislamu na
kuongeza kuwa: Tofauti na madai yao eti ya kupambana na makundi ya
kitakfiri, Wamarekani hawafanyi lolote la maana dhidi ya makundi hayo
bali baadhi ya ripoti zinaonesha kuwa, wanayasaidia.
3519154