IQNA

Wanaharakati wa Ghana kushiriki Tamasha la Kimataifa Imam Ridha AS

12:11 - August 10, 2016
Habari ID: 3470513
Wanaharakati watatu katika nyuga za dini, elimu na uchapishaji wanatazamiwa kushiriki katika Tamasha la 14 la Kimataifa la mjukuu wa Mtume SAW, Imam Ridha AS.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hayo yamebainika hivi karibuni katika mkutano uliofanyika, Accra, Ghana baina ya wanaharaki hao na mwambata wa utamaduni wa Iran Mohammad Hassan Ipakchi.

Akizungumza na wanaharakati hao, Bw. Ipakchi amesema ushiriki wa watatu hao ni fursa nzuri ya kuwawezesha kumfahamu kwa uzuri zaidi Imam Ridha AS na mbinu muafaka za kueneza mafundishi ya Ahul Bayt AS.

Katika kikao hicho, imependekezwa kuwa kuwepo mkakati maalumu wa kufuatilia maamuzi yaliyochukuliwa katika matamasha yaliyopita.

Tamasha la Kimataifa la Imam Ridha AS, litafanyika nchini Iran na kushirikisha nchi 77 mwaka huu.

Kati ya nchi zitakazoshiriki ni pamoja na Uganda, Tanzania, Madagascar, Mali, Myanmar, India, Bangladesh, China, Myanmar, Tajikistan na Georgia.

Halikadhalika kutakuwa na matamsha madogo katika maeneo 2400 kote duniani.

Tamasha la Kimataifa la Imam Ridha AS litaanza Agosti 11 katika mji mtakatifu wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.

3521562

Kishikizo: imam ridha as ghana iran
captcha