IQNA

Wanariadha waonyesha nguvu za Uislamu katika Olimpiki Rio

9:19 - August 18, 2016
Habari ID: 3470529
Wanariadha watatu Waislamu wameonyesha nguvu na taswira nzuri ya Uislamu katika michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, jarida la Time limechapisha taswira za baadhi ya wanariadha Waislamu ambao wamepata medali katika michezo ya Olimpiki inayoendelea mjini Rio nchini Brazil. Pamoja na kuwepo chuki dhidi ya Uislamu, wanariadha Waislamu wamewasilisha taswira nzuri katika michezo ya Rio.

Mohamed Farah Muingereza Mwenye asili ya Somalia, Sarah Ahmed wa Algeria na Ibtihaj Mohamed wametajwa na jarida la Time kuwa mfano wa wanariadha Waislamu ambao wametia for a katika Olimpiki pamoja na kuwepo ubaguzi na chuki dhidi ya Uislamu Rio.

Agosti 13, mwanariadah wa masafa marefu Mohamed Farah alikuwa anawania kulinda taji lake la Olimpiki la mbio za mita 10,000. Akiwa katikati ya mashindano, alianguka na kisha akainuka na kujipenyeza kati kati ya wanariadha wenzake na hatimaye akaibuka mshindi na kupata medali ya dhahabu.

Baada ya kupita mstari wa kumaliza mbio, Farah alisujudu hapo na kumshukuru Allah SWT kwa ajili ya ushindi huo. Hatua hiyo ya Farah kusujudu baada ya kumaliza mbio zilizokuwa zikitazamwa na makumi ya mamilioni ya watu kwa njia ya televisheni kote duniani ni jambo ambalo linaweza kuwasilisha taswira nzuri ya Uislamu. Kwa mtazamo wa Farah na wanariadha wengi Waislamu, kuwa na Imani ya Kiislamu ni sehemu ya mafanikio yao katika riadha. "Kwa kawaida mimi husoma Duaa kabla ya shindano lolote”, anasema Farah.

Hijabu katika Olimpiki

Wamagharibi wengi huwa na dhana potofu kuwa mwanamke Mwislamu mwenye kujisitiri kwa vazi la Hijabu anakandamizwa. Lakini mwanamke mwenye kunyanyua vyuma kutoka Misri, Sara Ahmed amethibtisha kuwa dhana hiyo si sahihi. Anaweza kunyanyua vyuma zaidi ya aghalabu ya wanawake duniani na ana nguvu ambazo ni wachache walizonazo. Akiwa amevalia hijabu yenye rangi za bendera ya Misri, Bi. Ahmed alinyanyua vyuma vyenye uzito wa kilo 255 kwa jumla na hivyo kupata medali ya shaba katika kategoria ya kilo 69.

Mafanikio hayo ni ya kipekee na hivyo ametajwa kuwa ni shujaa Misri kwani ni mwanamke wa kwanza nchini humo kupata medali katika historia ya miaka 104 ya michezo ya Olimpiki. Aidha ni mwanamke wa kwanza Mwarabu kupata medali ya Olimipki katika unyanyuaji vyuma.

Chuki dhidi ya Uislamu na Ubaguzi wa Rangi

Ibtihaj Mohamed alikuwa nyota ya jamii ya Waislamu Marekani hata kabla hajata umashuhuri duniani.

Kisa chake ni zaidi ya kuwa ‘mwanamke wa kwanza Mmarekani kushiriki katika michezo ya Olimpiki akiwa amevalia Hijabu.’

Alikuwa mtetezi haki ambazo zimepuuza na Waislamu na wasio kuwa Waislamu nazo ni haki za Wamarekani wenye asili ya Afrika na ambao ni Waislamu. Anasema kundi hili katika jamii ya Marekani hukabiliwa na tatizo la ubaguzi wa rangi sambamba na chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia. Akijibu matamshi ya mgombea urais kwa tikiti ya chama cha Republican, Donald Trump ambaye alitaka Waislamu watimuliwe Marekani alisema: "Mimi ni Mmarekani mwenye asili ya Afrika. Sina sehemu nyingine ya kwenda. Nimezaliwa na kulelewa New Jersey.”

Ibtihaj alipata nishani ya shaba katika mchezo wa vitara (fencing). Anasema ameshiriki katika Olympiki ili kuthibitisha kuwa, hakuna chochote kinachoweza kumzuia yeyote kufkia malengo yake, si rangi, dini au jinsia. "Nataka kuwa mfano hai kuwa, kila kitu kinawezekana kwa ustahamilivu," anasema Ibtihaj Mohamed. Mwenyeji huyo wa New Jersey anasema akiwa na umri wa miaka 13, alianza mchezo wa vitara.

Wanariadha waonyesha nguvu za Uislamu katika Olimpiki Rio

Mohammad Farah kutoka Uingereza  akisujudu baada ya kushinda medali ya dhahabu

Wanariadha waonyesha nguvu za Uislamu katika Olimpiki Rio

Sarah Ahmed mshindi wa medali ya shaba kutoka Misri katika unyanyuaji vyuma

Wanariadha waonyesha nguvu za Uislamu katika Olimpiki Rio
Sarah Ahmed mshindi wa medali ya shaba kutoka Misri katika unyanyuaji vyuma

Wanariadha waonyesha nguvu za Uislamu katika Olimpiki Rio
Ibtihaj Mohammad, Mmarekani mshindi wa nishani ya shaba katika mchezo wa vitara (fencing)

3523567

captcha