IQNA

Bondia Mwislamu Marekani apigwa marufuku kwa ajili ya Hijabu

18:58 - November 23, 2016
3
Habari ID: 3470693
IQNA- Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limebainisha masikitiko yake baada ya bondia wa kike Mwislamu kupigwa marufuku Marekani kwa ajili ya vazi lake la Kiislamu la Hijabu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Bi. Amaiya Zafar kutoka Oakdale, jimboni Minnesota, alizuiwa dakika ya mwisho kushiriki katika mashindano ya ndondi ya Bert Boxing National Championships yaliyokuwa yakifanyika Novemba 20 katika eneo la Kissimmee jimboni Florida,

Mama yake binti huyo aliliropiti tukio hilo la kibaguzi kwa CAIR, taasisi ambayo hutetea haki za Waislamu Marekani, na kusema binti yake alijisajili, kupimwa wizani na kuvaa glovu zake na hata kuingia ugani lakini hapo afisa moja wa mashindano akamfahamisha kuwa hawezi kushiriki akiwa amevaa Hijabu. Mshindani wake ambaye hakufuriahishwa na tukio hilo alimkabidhi Zafar mshipi aliopewa na waandalizi waliokuwa wamemtangaza 'mshindi'.

Msemaji wa CAR Ibrahim Hopper amelaani tukio hilo na kusema wanamichezo wote wanapaswa kuruhusiwa kushiriki katika mashindano pasina kuwepo vizingiti vya kibaguzi ambavyo vimepitwa na wakati. Aidha amemshukuru bondia aliyemkabidhi Zafar mshipi huo kama njia ya kufungamana naye kufuatia tukio hilo la ubaguzi.

Hopper aidha ametoa wito kwa Shirikisho la Kimataifa na Ndondi (AIBA) na Shirikisho la Ndondi la Marekani kuruhusu Hijabu ili wanamasumbwi wa kike kama Zafar washiriki pasina kuwepo vizingiti.

Mashirika mengi ya riadha yamepasisha sheria za kuwaruhusu wanawake Waislamu kushuriki katika michezo wakiwa wamevaa Hijabu. Shirika la Soka Duniani FIFA na Shirika la Kimataifa la Wanyanyua Vyuma IWF ni katika ya mashirika ya kimataifafa ya michezo ambayo yameondoa marufuku ya sare za Hijabu kwa wanawake Waislamu.

3461506

Imechapishwa: 3
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
muhideen ali
0
0
Ulimwengu lazima ibadilike.
Hii tabia za ubaguzi sio nzuri.
muhideen ali
0
0
Ulimwengu lazima ibadilike.
Hii tabia za ubaguzi sio nzuri.
Salim Mohamed
0
0
Hivi Bado Mna Chuki Na Waislam!? Badilikeni Jama.
captcha