IQNA

Waislamu London wagawa misaada ya chakula wakati wa Krismasi

13:49 - December 19, 2016
Habari ID: 3470749
IQNA: Waislamu katika mji mkuu wa Uingereza, London wamekusanya tani nyingi za chakula kwa ajili ya kuwasaidia mayatima na watoto wa mitaani katika kipindi hiki cha sherehe za kufunga mwaka.

Shirika la Muslim Aid kwa ushirikiano na usimamizi wa Msikiti wa London Mashariki wamekusanya misaada ya chakula katika eneo laWhitechapel, kwenye viungavya mji wa London, kwa ajili ya kuwapa watoto yatima hususan Wakristo.

Dilowar Khan, Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Msikiti wa London Mashariki amesema, asilimia 90 ya misaada hiyo watapewa mayatima Wakristo, haswa kwa kuzingatia wafuasi wa dini hiyo wanatazamiwa kusherehekea Krismasi yaani kumbukumbu ya mazazi ya Nabii Issa Masih AS.

SheikhAbdul Qayum, Imamu Mwandamizi wa Msikiti wa London Mashariki amesema, Waislamu wametoa misaada hiyo kwa wingi kwa kuwa dini yao inawafundisha kuwa wepesi wa kusaidia pasi na kujali imani na itikadi zao.

Naye Ian Richards, Mkuu wa shirika la Crisis at Christmas, amewashukuru Waislamu wa mji wa London kwa kutoa misaada hiyo kwa ajili ya mayatima na watoto wa kurandaranda mitaani wa mji huo.

Hii ni katika hali ambayo, mji huo mkuu wa Uingereza, siku ya Jumamosi ulikuwa mwenyeji wa mkutano uliofanyika chini ya anuani ya "Mazingira ya Chuki na Utawala wa Kipolisi"mkutano ambao ulihudhuriwa na wasomi wa vyuo vikuu na waandishi wa vyombo vya habari wa Uingereza, nchi nyingine za Ulaya pamoja na Marekani.

Mkutano huo ulioandaliwa na Kamisheni ya Kiislamu ya Haki za Binadamu yenye makao yake mjini London imechunguza mbinu na mifano hai ya uenezaji chuki dhidi ya Uislamu, ubaguzi wa rangi na vilevile sababu ya kuongezeka chuki na hofu juu ya Uislamu katika ulimwengu wa Magharibi.

3461700

captcha