IQNA

Brazil yailaani Israel kwa kujenga vitongoji katika ardhi za Palestina

17:29 - April 05, 2017
Habari ID: 3470919
TEHRAN (IQNA) Brazil imeulaani utawala wa Israel kwa kuidhinisha ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazil imetoa taarifa na kulaani uamuzi uliopasishwa hivi karibuni na baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuidhinisha ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Taarifa hiyo imesema kuwa, upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu mbali na kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa, lakini pia unazidi kuvuruga kile kinachotajwa kama mchakato wa kuundwa nchi mbili ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Palestina na Israel.

Wizarahiyo imesisitiza kuhusu msimamo wa serikali ya Brazil wa kutaka kuundwa taifa huru la Palestina kwa misingi ya michoro ya mipaka ya mwaka 1967.

Haya yanajiria siku chache baada yaWizara ya Mambo ya Nje ya Misri kutoa taarifa kama hiyo na kulaani hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuidhinisha ujenzi wa nyumba mpya za walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Disemba lilipasisha azimio la kutaka kusimamishwa mara moja ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Azimio hilo ambalo ni lakwanza kupasishwa na Baraza la Usalama dhidi ya Israel katika kipindi cha miaka minane, liliungwa mkono kwa kura 14, huku nchi moja pekee ikijizuia kupiga kura.

3462505

captcha