IQNA

Bondia wa kike Mwislamu Marekani ashinda haki ya kuvaa Hijabu+PICHA

15:07 - May 04, 2017
1
Habari ID: 3470967
TEHRAN (IQNA)- Bondia wa kike Mwislamu nchini Marekani ameweka historia na kuwa wa kwanza kushiriki katika mchezo rasmi wa masumbwi akiwa amevaa Hijabu.

Bi.Amaiya Zafar amekuwa akitetea haki yake ya kuvaa Hijabu wakati akiwa katika mchezo wa masumbwi na hatimaye amefanikiwa. Zafar aliweka historia Jumamosi Aprili 29 wakati aliposhiriki katika mashindano rasmi ya Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Marekani (USA Boxing) . Idadi kubwa ya watu walifika kutizama pigano hilo katika Shule ya Msingi ya Richard R. Green huko Minneapolis ili washuhudie historia ya mshiriki wa kwanza aliyevaa hijabu katika mchezo rasmi wa masumbwi nchini Markeani. Ingawa Zafar hakushinda pigano hilo, lakini alisema hilo si muhimu bali muhimu zaidi ni kuweza kuvaa Hijabu kwa mafundisho ya dini yake ya Kiislamu.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) Tawi la Minnesota limesema sheria mpya ya kuruhusu wanamasumbwi wanawake kuvaa hijabu inatazamiwa kupitishwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa mwezi Juni.

Binti huyo mwenye umri wa miaka 16 anasema analenga kushiriki katika Mashindano ya Olimpiki Tokoyo mwaka 2020.

Novemba mwaka jana Bi. Zafar alizuiwa dakika ya mwisho kushiriki katika mashindano ya ndondi ya Bert Boxing National Championships yaliyokuwa yakifanyika jimboni Florida.

Mama yake binti huyo aliliropiti tukio hilo la kibaguzi kwa CAIR, taasisi ambayo hutetea haki za Waislamu Marekani, na kusema binti yake alijisajili, kupimwa wizani na kuvaa glovu zake na hata kuingia ugani lakini hapo afisa moja wa mashindano akamfahamisha kuwa hawezi kushiriki akiwa amevaa Hijabu. Mshindani wake ambaye hakufuriahishwa na tukio hilo alimkabidhi Zafar mshipi aliopewa na waandalizi waliokuwa wamemtangaza 'mshindi'.

Mashirika mengi ya riadha yamepasisha sheria za kuwaruhusu wanawake Waislamu kushuriki katika michezo wakiwa wamevaa Hijabu. Shirika la Soka Duniani FIFA na Shirika la Kimataifa la Wanyanyua Vyuma IWF ni katika ya mashirika ya kimataifa ya michezo ambayo yameondoa marufuku ya sare za Hijabu kwa wanawake Waislamu.


 
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Luqmaantenrec
0
0
UJASIRI MKUBWA KATIKA UGA WAMISHEZO. ILA KWETU DRC TUNA BAGULIWA.
captcha