IQNA

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani Barani Ulaya watangazwa

11:21 - September 11, 2017
Habari ID: 3471166
TEHRAN (IQNA)- Mashidano ya 5 ya Qur'ani Tukufu yemamalizika Stockholm nchini Sweden Jumapili kw akutangazwa washindi.

Mashindano hayo yalifanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Imam Ali AS mjini Stocholm baada yay a kumalizika duru ya mwisho ya mashindano hayo.

Akizungumza na IQNA, Sheikh Muhsin Ilahi, mkurugenzi wa kituo hicho cha Kiislamu amesema Mohammad Mohammadi kutoka mji wa Malmo, Sweden, alichukua nafasi ya kwanza katikakategoria ya qiraa ya Qur'ani Tukufu ya watu wazima. Naye Seyed Abbas Ali kutoka Hamburg, Ujerumani, ameshika nafasi ya pili huku Mohammad Mohsen Jafari wa Stockholm, akichukua nafasi ya tatu.

Katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani Fazil al-Imara wa Sweden ameibuka mshini naye Hudaa Ahmadi, pia kutoka Sweden ameshika nafasi ya kwanza katika kategoria ya ufahamu wa Qur'ani. Kategoria hii ilikuwa maalumu kwa ajili ya wanawake.

Katika mashindano ya Adhana, Qadir Maftuhu kutoka Milan Italia ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Saeed Akbari kutoka Denmark na Hassan Fahim kutoka Helsinki Finland alishika nafasi ya tatu.

Mashindano ya mwaka huu ya Qur'ani Tukufu barani Ulaya yalianza Ijumaa na yalijumuisha washiriki kutoka nchi za Sweden, Norway, Finland, Denmark, Italia na Ujerumani.

Mashindano hayo yalisimamiwa na majaji wataalamu wa Qur'ani na washindi wanatazamiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwakani.

Mwaka jana mashindano hayo yalikuwa na washiriki 92 kutoka Sweden, Norway, Denmark na Finland ambapo majaji walikuwa ni kutoka Denmark, Iran, Sweden, Ujerumani na Uholanzi.

Waandalizi wa mashindano hayo wanasema kati ya malengo yao ni kustawisha utamaduni wa Qur'ani, kuhumiza umoja wa Kiislamu na kubaini vipawa na vipaji vya Qur'ani mioni mwa vijana Waislamu barani Ulaya.

3463876


captcha