IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu ya mchezaji wa zamani wa Arsenal+Video

11:34 - October 26, 2017
Habari ID: 3471231
TEHRAN (IQNA)-Klipu ya video imeenea katika mitandao ya kijamii ikumuonyesha mchezaji wa zamani wa Timu ya Soka ya Arsenal ya Uingereza, Vassiriki Abou Diaby akisoma Qur'ani Tukufu.
Qiraa ya Qur'ani Tukufu ya mchezaji wa zamani wa Arsenal+VideoKlipu hiyo inamuonyesha Abou Diaby, ambaye pia aliwahi mkuwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Soka ya Ufaransa, akisoma Qur'ani kwa mbinu ya Tartil.

Abou Diaby anasikika akisoma aya za 11 hadi 14 za Sura Taha kwa kuzingatia kanuni za usomaji Qur'ani.

Inaaminika kuwa klipu hiyo ya video inahusiana na msimu wa Hija wa mwaka 1438 Hijria Qamaria katika moja ya maheama ya eneo la Mina.

Abou Diaby alipata umaarufu kama mchezaji wa Ligi ya Premier ya England ambaye alikuwa amehifadhi Juzuu 19 za Qur'ani Tukufu. Tizama kilipu ya video hapo chini.

3656975/




captcha