IQNA

Idhaa ya Qur'an Tunisia yapigwa marufuku kwa kueneza itikadi za ukufurishaji

11:25 - November 04, 2017
Habari ID: 3471247
TEHRAN (IQNA)-Idhaa ya Qur'ani nchini Tunisia imesitisha matangazo yake baada ya serikali ya nchi hiyo kuipiga marufuku kutokana na kueneza itikadi za ukufurishaji.

Taarifa zinasema, Hisham Sanousi, mwanachama wa Tume ya Kuratibu Vyombo vya Habari amesema, Radio ya Qur'ani pia imefungwa kwa sababu ya kuendesha matangazo pasina kuwa na kibali. Aidha amesema tume hicho imechukua udhibiti wa vifaa vyote vya idhaa hiyo ya Qur'ani.

Sanousi amesema moja ya masharti ya kibali cha vyombo vya habari nchini humo ni kuwa wamiliki wasiwa na nafasi au cheo cha kisiasa. Hii ni katika hali ambayo, Saeed Jaziri, mmiliki wa Radio ya Qur'ani pia ni kiongozi cha chama cha kisiasa cha al-Rahma.

Sanousi pia amekosoa vikali vipindi vya idhaa hiyo na kusema baadhi ya vipindi vyake vimekuwa vikieneza itikadi za Kiwahhabi za kuwakufurisha Waislamu wengine.

Tunisia imekuwa ikikabiliana na tatizo la magaidi wenye fikra za ukufurishaji ambao wametekeleza mashambulizi mara kadhaa katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini na wakuu wa nchi hiyo wanatekeelza kampeni maalumu ya kukabiliana na tatizo hilo.

/3659705/

captcha