IQNA

Kiongozi asisitiza kusaidiwa walioathirika na tetemeko la ardhi Iran

9:10 - November 15, 2017
Habari ID: 3471264
Tehran (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia mshikamano wa viongozi kwa wahanga wa tetemeko la ardhi katika ngazi ya utendaji sambamba na kuendelea kutolewa misaada kwa watu hao ili kuweza kupunguza matatizo yao.
Kiongozi asisitiza kusaidiwa walioathirika na tetemeko la ardhi IranAyatullahil-Udhma Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Kiongozi Muadhamu ameyasema hayo Jumanne mjini Tehran katika kikao na viongozi wa mihimili mitatu ya dola, yaani vyombo vya mahakama, bunge na serikali kuu.
Sambamba na kuonyesha masikitiko yake kutokana na ukubwa wa tukio hilo chungu la tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Kermanshah, amelitaja tukio hilo kuwa mtihani wa Mwenyezi Mungu.
Kiongozi Muadhamu ameashiria hatua ya viongozi akiwemo Rais Hassan Rouhani ya kufika miongoni mwa wahanga wa tukio hilo na kuwapa pole na matumaini na kussisitiza mshikamano huo katika uga wa utendaji na kuwasaidia wahanga kwa nguvu zao zote, ili kuweza kuwapunguzia matatizo yao. Ameashiria hali inayoshuhudiwa ya huruma, mapenzi na kusaidiana kunakoshuhudiwa katika jamii ya Kiislamu yalivyokuwa na taathira katika tukio hilo na kusema, tukio hilo la tetemeko la ardhi limewafanya watu wote kuingia katika ulingo wa kusaidia waathirika na kutaraji kwamba athari ya mapenzi hayo na udugu na kwa baraka za Mwenyezi Mungu, zitashamili kati ya wakazi wote wa Kermanshah na kwa taifa lote la Iran.Kiongozi asisitiza kusaidiwa walioathirika na tetemeko la ardhi Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kubainisha kwamba Wairan wote wanashirikiana katika msiba huu na watu majasiri na walinda mpaka shupavu wa mkoa wa Kermanshah, amesema, msiba huu na kuondokewa watu wao wa karibu ni mchungu sana, lakini anataraji kwamba Mwenyezi Mungu atashusha utulivu katika mioyo ya watu wa familia zilizoondokewa na wapenzi wao.
Tetemeko la ardhi lililokuwa la ukubwa wa 7.3 kwa kipimo cha Rishta lilitokea siku ya Jumapili usiku katika maeneo mbalimbali ya magharibi mwa Iran  na pia katika maeneo ya mashariki mwa Iraq. Hadi kufikia sasa karibu watu 500 wameaga dunia na wengine, elfu saba kujeruhiwa katika zilzala hiyo.

3663536
captcha