IQNA

Waislamu Uingereza waanzisha kampeni dhidi ya ugaidi

14:04 - January 22, 2018
Habari ID: 3471366
TEHRAN (IQNA)-Baraza la Waislamu Uingereza (MCB) limetangaza kuanzisha mpango mpya wa kukabiliana na ugaidi.

Katika mkutano uliofanyika London Kaskazini siku ya Jumamosi, baraza hilo limezindua kampeni hiyo ya kukabiliana na ugaidi katika fremu ya kongamano la kwanza la 'Misikiti Yetu, Mustakabali Wetu."

Katibu Mkuu wa MCB Harun Khan amesema mpango huo umejengeka katika msingi wa kufanya mazungumzo na jamii zote za Waislamu nchini Uingereza ambapo zaidi wakuu wa baraza hilo watajikita katika kusikiliza maoni.

Baraza hilo linasema litasikiliza sauti za Waislamu mashinani na namna walivyoathiriwa na sheria za serikali za kupambana na ugaidi na kuangalia dosari zilizopo.

Mmoja wa wahusika wakuu wa MCB katika mpango huo, Asif Hussain, anasema hawalengi kuchukua nafasi ya serikali katika vita dhidi ya ugaidi bali kile wanacholenga kufanya ni kuitaka serikali kufanya mazungumzo na jamii athirika. Aidha amesema kuna haja ya kujadiliana kuhusu maana ya misimamo mikali ya kidini na Waislamu wahusishwe kikamilifu katika kubainisha maana ya msamiati huo.

3684250/

captcha