IQNA

Washindi wa Mashindano ya Qur’ani Ulaya watunukiwa zawadi

21:55 - March 09, 2018
Habari ID: 3471423
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Hamburg kimetangaza washindi wa Mashindano ya Sita ya Kimataifa ya Qur’ani ya Waislamu wa Ulaya.

TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Hamburg kimetangaza washindi wa Mashindano ya Sita ya Kimataifa ya Qur’ani ya Waislamu wa Ulaya.

Mashindano hayo yaliandaliwa na Kitengo cha Darul Qur’an al Karim katika kituo hicho kuanzia Machi 2-4 ambapo kulikuwa na Waislamu zaidi ya 170 walioshiriki kutoka nchi za Ulaya zikiwemo Ujerumani, Denmark, Belgium, Uingereza, Ureno, Italia, Sweden, Ufaransa, Austria na Uholanzi.

Mashindano hayo yalikuwa na vitengo viwili vya wanaume na wanawake waliokuwa katika makundi ya maborobaro na watu walio na umri wa zaidi ya miaka 20.

Halikadhalika mashindano hayo yalikuwa na kategoria za qiraa, kuhifadhi Qur’ani, Adhana na ufahamu wa Qur’ani.

Kati ya washindi katika mashindano hayo ni Mohammad Mohammadi, Mohammad Ridha Nurullahi na Sayyid Hamza Hussein kwa taratibu katika kitengo cha qiraa. Washindi wa kategoria ya kuhifadhi Qurani walikuwa ni pamoja na Batul Hussein wa Ujerumani, Rana Hamza wa Sweden na Ghani Hassan wa Ujerumani.

Mashindano hayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kueneza utamaduni wa Qur’ani na pia kutambua vipaya vya Qur’ani miongoni mwa Waislamu barani Ulaya.

3697931

 

captcha