IQNA

Baraza la Kimataifa la Wahudumu wa Qur'ani laundwa Misri

18:35 - March 25, 2018
Habari ID: 3471443
TEHRAN (IQNA)-Baraza la Kimataifa la Wahudumu wa Qur'ani Tukufu limeasisiwa nchini Misri katika kikao kilichohudhuriwa na wataalamu na wanaharakati wa Qur'ani.

Taarifa kuhusu kuundwa baraza hilo imetangazwa na Waziri wa Wakfu nchini Misri Sheikh Mohammad Mokhtar Gomaa. Akifafanua Zaidi Sheikh Gomaa amesema: " Baraza la Kimataifa la Wahudumu wa Qur'ani Tukufu litawajumuisha majaji wote waliowahi kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya wizara ya wakfu Misri."

Aidha amesema katiak siku za usoni baraza hilo litawajumuisha wale wote walio katika harakati za Qur'ani nchini Misri na maeneo mengine duniani. Amesema maelezo Zaidi kuhusu baraza hilo yatatangazwa baada ya kumalizika Mashindano ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Misri.

Mashindano hayo yalianza Jumamosi na yataendelea hadi siku ya Alhamisi yanalenga pia kusitiza umoja wa Waislamu katika kuitetea Quds Tukufu.

3701903

captcha