IQNA

Mtoto mwenye ulemavu wa macho ahifadhi Qur'ani kwa Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa

13:53 - April 01, 2018
1
Habari ID: 3471450
TEHRAN (IQNA)-Mtoto mwenye ulemavu wa machi Misri amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamlifu kwa lugha asi ya Kiarabuna pia kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa.

Mtoto huyo kwa jina la Abdullah Amar Mohammad Al Sayyid amewashangaza wengi kwani hawakutarajia kuwa angeweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu kwa lugha hizo tatu kutokana na ulemavu wake wa macho.

Mbali na hayo, mtoto huyo mwenye kipaji pia amehifadhi nambari ya kurasa anazosoma.

Kutokana na motisha aliyopata kutoka kwa baba yake na pia waalimu wake wawili binafsi, mtoto huyo pia sasa ana uwezo wa kubainisha maana ya aya kwa lugha za Kifaransa na Kingereza.

Amar Mohammad Al Sayyid alienziwa na Waziri wa Wakfu Misri Sheikh Mokhtar Gomaa katika katika Mashindano ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yaliyofanyika hivi karibuni mjini Cairo.

Miaka miwili iliyopita, Sheikhe Mkuu wa Al Azhar Ahmad Tayyib aliahidi kumsomesha mtoto huyo hadi kufikia kiwango cha shahada ya uzamivu.

/3702522

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bila jina
0
0
MAASHAALAH
captcha