IQNA

Al Azhar Imetayarisha Tarjuma Mpya ya Qur'ani kwa Lugha ya Kiswahili

15:32 - April 04, 2018
Habari ID: 3471453
TEHRAN (IQNA)-Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri imetangaza kukamilika tarjuma mpya ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili.

Mkuu wa Idara ya Tarjuma katika chuo hicho, Sheikh Yusuf Amer amesema kuna mpango wa kuandika tarjuma 30 mpya za Qur'ani Tukufu na tayari tarjuma za lugha kadhaa zimeshakamilika.

Akizungumza kuhusu warsha kuhusu "Nafasi ya Al-Azhar Katika Kustawisha Utamaduni wa Kiislamu," iliyofanyika pembizoni mwa Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Alexandria, alisema, "tarjuma mpya za Qur'ani Tukufu kwa lugha za Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili tayari zimeshakamilika."

Halikadhalika amesema wana mpango wa kuchapisha tarjuma ya tafsiri ya Qur'ani ya Shaykh Muhammad Mutawalli al-Sha'rawi kwa lugha kadhaa.

Sheikh Amer ameongeza kuwa Idara ya Tarjuma ya Al Azhar pia iko mbioni kuchapisha kamusi ya istilahi za Kiislamu. Maonyesho ya 14 ya Kimataifa ya Vitabu ya Alexandria yalianza  Machi 31 na yataendelea hadi Aprili 9.

3702694

 

captcha