Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam Ali Mohammadi, Mkuu wa Shirika la Wakfu la Iran katika mahojiano na IQNA huku akiongeza kuwa kutakuwa mashindano manne tafauti ya Qur;ani katika duru ya mwaka huu.
Amesema mbali na mashindano ya kawaida kutakuwa na mashindano maalumu ya wanawake, wanafunzi wa shule na pia mashindano maalumu ya wenye ulemavu wa macho. Halikadhalika amesema kwa ujumla mashindano yam waka huu yatakuwa na washiriki zaidi ya 300.
Hujjatul Islam Ali Mohammadi pia amesema kuna mpango wa kuandaa kongamano la kimataifa la utafiti wa Qur'ani ambapo mada kuu itakuwa namna ya kupambana na uistikbari kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu na Sirah ya Ahul Bayt AS.
Aidha ameashiria kuhusu mpango wa kuhifadhi Qur'ani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema hadi sasa watu milioni 2 wamejisajili kushiriki katika mpango huo wa kitaifa ambao unasimamiwa na Shirika la Wakfu la Iran.