IQNA

Nchi 83 Kushiriki Mashindano ya Qur'ani Nchini Iran

19:06 - April 06, 2018
Habari ID: 3471455
TEHRAN (IQNA)-Nchi 23 zimetangaza azma ya kushiriki katika Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baadaye mwezi huu.

Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam Ali Mohammadi, Mkuu wa Shirika la Wakfu la Iran katika mahojiano na IQNA huku akiongeza kuwa kutakuwa mashindano manne tafauti ya Qur;ani katika duru ya  mwaka huu.

Amesema mbali na mashindano ya kawaida kutakuwa na mashindano maalumu ya wanawake, wanafunzi wa shule na pia mashindano maalumu ya wenye ulemavu wa macho. Halikadhalika amesema kwa ujumla mashindano yam waka huu yatakuwa na washiriki zaidi ya 300.

Hujjatul Islam Ali Mohammadi pia amesema kuna mpango wa kuandaa kongamano la kimataifa la utafiti wa Qur'ani ambapo mada kuu itakuwa namna ya kupambana na uistikbari kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu na Sirah ya Ahul Bayt AS.

Aidha ameashiria kuhusu mpango wa kuhifadhi Qur'ani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema hadi sasa watu milioni 2 wamejisajili kushiriki katika mpango huo wa kitaifa ambao unasimamiwa na Shirika la Wakfu la Iran.

3703287

captcha