IQNA

CAIR: Trump Amechangia Kuongeza Chuki dhidi ya Uislamu Marekani

16:04 - April 18, 2018
1
Habari ID: 3471470
TEHRAN (IQNA) - Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani (CAIR) limetangaza ripoti ambayo ina ushahidi unaoonyesha kuwa hatua ya utawala wa Rais Donald Trump kupiga marufuku Waislamu kutoka baadhi ya nchi kuingia nchini humo ni jambo ambalo limechangia kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.

Taarifa ya mwaka 2018 ya CAIR ambayo itazinduliwa rasmi Aprili 23 imeorodhesha mamia ya matukio ya ubaguzi na chuki dhidi ya Waislamu katika mwaka uliopita wa 2017.  Ripoti hiyo inaonyesha namna vitendo hivyo inahusika na tangazo la Trump lililokiuka katiba la kuwapiga marufuku raia wan chi sita zenye Waislamu wengi kuingia nchini humo.

Itakumbukwa kuwa tarehe 25 ya mwezi Septemba mwaka 2017 Rais Donald Trump wa Marekani alitoa amri mpya dhidi ya uhajiri kwa kuwawekea vizuizi vikali zaidi kulinganisha na hapo kabla vya kuingia nchini Marekani raia wa nchi zenye Waislamu wengi za Chad, Iran, Libya, Somalia, Syria, Yemen na pia madola mengine mawili yasiyo ya Kiislamu yaani Korea Kaskazini na Venezuela.

Ripoti hiyo yenye anuani ya "Waliolengwa" pia inasema utawala wa Trump unawalenga kwa makusudi Waislamu raia wa Marekani, amesema Mkurugenzi Mkuu wa CAIR Nihad Awad.  CAIR inasema uchunguzi wake umebaini kuongezeka chuki lisilo na kifani la chuki dhidi ya Waislamu na watu wa jamii nyinginezo za wachahce nchini humo tokea Trump aingie madarakani Januari 2017.

CAIR hivi sasa mpango wa kutoa mafunzo maalumu ya njia za kukabiliana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.

3465582

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
ANU ABDU
0
0
A/MALLEKUM NDUGU ZANGUNI NA KAKA ZANGUNI OMBI LANGU NKITAKA MUNIPE HABARI JAPO KWA UFUPI KWENYE NAMBA YANGU HII YA WHATSAP 0773 434368 AHSANTENI
captcha