IQNA

10:37 - May 20, 2018
News ID: 3471522
TEHRAN (IQNA)- Duru ya 25 ya Mashidano ya Qur’ani ya Watoto wa kike na kiume yameanza nchini Qatar Mei 18.

Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo ambayo ni maarufu kama ‘Mashindano Sheikh Jasim bin Muhammad’ yanawajumuisha watoto 2300 wakiwemo Waqatari na wan chi za kigeni wanaoishi nchini humo.

Mashindano hayo ambayo yameandaliwa kwa munasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yanatazamiwa kuendelea kwa muda wa siku saba.

Waandalaizi wa mashindano hayo ya Qur’ani wanasema mwaka huu kuna washiriki 200 zaidi ya mwaka jana. Kuna majaji 18 wataalamu wa Qur’ani wanaosimamia mashindano hayo. Nchi ya Qatar iliyo katika Ghuba ya Uajemi inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 2.6 wakiwemo raia wa kigeni na huandaa mashindano mengi ya kitaifa na kimataifa ya Qur’ani Tukufu.

3715305

Name:
Email:
* Comment: