IQNA

11:07 - May 20, 2018
News ID: 3471523
TEHRAN (IQNA)-Duru ya 26 ya Maonyesho ya 26 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu yamefunguliwa Jumamosi jioni.

Maonyesho hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Sala (Musalla) wa  Imam Khomeini MA mjini Tehran na sherehe za ufunguzi zimehudhuriwa na wanazuoni, wataalamu wa Qur’ani na wahusika wa harakati za Qur’ani Tukufu nchini Iran.

Aidha katika sherehe hizo kulikuwa na ujumbe maalumu wa video kutoka kwa Ayatullah Jaafar Subhani ambaye alisisitiza umuhimu wa kufanya utafiti na kuzingatia mafundisho ya Qur’ani Tukufu ili kubaini siri zisizo na kikomo katika kitabu hicho kitukufu.

Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho hayo, Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran Sayyed Abbas Salehi amesistiza umuhimu wa kueneza mafundisho ya Qur’ani katika jamii ili mafundisho hayo yaweze kutekelezwa kivitendo. Katika maonyesho hayo pia kulizinduliwa nakala nadra ya Qur’ani Tukufu inayonasibiwa na Imam Ali AS.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur’ani Bw. Abdu Hadi Faqihzadeh, maonyesho hayo ya wiki mbili yatakuwa na shughuli kadhaa ikiwa ni pamoja na washa.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu kwa lengo la kustawisha uelewa wa Qur’ani na kuimarisha harakati za Qur’ani nchini.

Maonyesho hayo kwa kawaida huwa sehemu ya kuwasilisha amfnaikio ya hivi karibuni katika sekta ya Qur’ani nchini Iran nan chi zingine duniani.

/3715800

Maonyesho ya 26 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran Yazinduliwa

Maonyesho ya 26 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran Yazinduliwa

Maonyesho ya 26 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran Yazinduliwa

Name:
Email:
* Comment: