IQNA

14:47 - May 23, 2018
News ID: 3471528
TEHRAN (IQNA)- Kwa munasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Uturuki imetangaza kusambaza nakala 55,000 za Qur'ani Tukufu katika maeneo mbali mbali duniani.

Kwa mujibu wa Abdurrahman Cetin Naibu Mkuu wa Taasisi ya Diyanet (TDV) ambayo ni taasisi ya serikali ya Uturuki inayoshughulikia masuala ya kidini, amesema nakala hizo za Qur'ani Tukufu zinasambazwa katika nchi 17 duniani. Aidha amesema nakala hizo za Qur'ani zilizosambazwa zina tarajama za lugha 10 za maeneo mbali mbali ya dunia.

Taasisi hiyo imesema nakala hizo 55,000 za Qur'ani zimesambazwa miongoni mwa Waislamu katika nchi za  Sri Lanka, Colombia, El Salvador, Guatemala, Belize, Haiti, Panama, Chile, Ecuador, Peru, Malawi, Zimbabwe, Ghana, Kazakhstan, Jamhuri Yenye Mamlaka ya Ndani ya Nakhchivan, Syria na Kenya.

Halikadhalila amesema nakala hizo za Qur'ani zina tarjama ya lugha za Kituruki, Kifaransa, Kiingereza, Kihispania, Kikazakh, Kiazeri, Chichewa, Kitamil na Kikurdi mbali na lugha asili ya Kiarabu.

Halikadhalika Cetin amaesema Taasisi ya Diyanet imeandaa futari katika maeneo 326 katika nchi 84 duniani.

3716901

Name:
Email:
* Comment: