IQNA

12:24 - May 31, 2018
News ID: 3471538
TEHRAN (IQNA)- Washindi wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani nchini Sierra Leonne wametunukiwa zawadi katika sherehe iliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Iran katika mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yaliandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Iran kuanzia Mei 26-27.

Washindi wa nafasi tatu za kwanza katika kategoria za kusoma na kuhifadi Qur'ani kikamilifu, Juzuu 10 na pia tafsiri kwa lugha ya Creole ya Sierra Leone walipata zawadi katika sherehe hiyo.

Akizungumza katika halfa hiyo mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Freetown Alireza Farmarzi amesema lengo kuu la mashindano hayo ni kuwawezesha washiriki kufahamu kwa kina mafundisho ya Qur'ani na kisha wayatekeelza maishani.

Naye Dkt. Maithamzadeh, mkurugenzi wa tawi la Sierra Leone la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa  amezungumza katika mahafali hiyo na kusisitiza muhimu wa kufuata Sirah ya Mtume SAW na Ahul Bayt AS katika kutekeelza mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

3718641/

Name:
Email:
* Comment: