IQNA

Maandamano ya Kimataifa ya Siku ya Quds Kote Duniani Kuunga Mkono Palestina

22:27 - June 08, 2018
Habari ID: 3471547
TEHRAN (IQNA)- Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds (Jerusalem) yamefanyika leo kote duniani kwa lengo la kuunga mkono ukombozi wa Palestina na kulaani utawala ghasibu wa Israel.

Katika uwanja huo maandamano ya Siku ya Quds yameshuhudiwa katika nchi mbalimbali kuanzia Asia, Afrika, Ulaya hadi Marekani. Mjini Moscow, Russia Waislamu na wanaharakati wameshiriki kongamano kubwa katika msikiti mkuu wa mji huo na katika mitaa ya karibu katika kupaza sauti na kulaani jinai na dhulma za utawala khabithi wa Kizayuni. Katika kongamano hilo mabalozi wa nchi 12 wanaoziwakilisha nchi zao nchi Russia kuanzia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Uturuki, Iraq, Afghanistan, Lebanon, Pakistan, Nigeria, Misri, Kazakhstan, Azerbaijan, Tajikistan na Syria wameshiriki.

Sheikh Rawil Gaynetdin, Mkuu wa Baraza la Mamufti nchini Russia amesema kuwa, Siku ya Quds ni turathi yenye  thamani kubwa iliyobuniwa na Imamu Khomeini MA Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ameashiria hatua ya kichokozi ya Marekani ya kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Quds na kuongeza kuwa, hatua hiyo ambayo ilitekelezwa sambamba na kufanyika mauaji ya kinyama dhidi ya Wapalestina, imezidisha chuki dhidi ya Marekani na utawala katili wa Kizayuni sambamba na kuonyesha udharura wa kushikamana na raia wa Palestina.

Siku ya Quds barani Afrika

Waislamu na wanaharakati wa haki za binaadamu wa nchi za Afrika nao hawakuachwa nyuma katika kutangaza uungaji mkono wao kwa raia madhlumu wa Palestina. Katika uwanja huo, miji ya Afrika Mashariki ya Dar es Salaam,  Nairobi, Bujumbura na kwengineo imeshuhudiwa maandamano hayo. Kadhalika nchi za Afrika Magharibi kuanzia Nigeria, Senegal Mali nk nazo pia zimeshuhudia maandamano makubwa ya kuwaunga mkono Wapalestina.

Katika maandamano hayo washiriki wamepiga nara kutangaza uungaji mkono wao kwa taifa la Palestina na kulaani jinai za utawala katili wa Kizayuni. Aidha wametangaza kwamba, mji wa Quds ni mji mkuu wa Palestina na utaendelea kubakia hivyo. Hayo yanajiri katika hali ambayo mamilioni ya watu nchini Iran wameadhimisha siku hiyo kwa kufanya maandamano makubwa katika miji yote ya nchi hii. Mjini Tehran waandamanaji wamelinyonga sanamu la Rais Donald Trump wa Marekani ambapo sambamba na kuitaja nchi hiyo kuwa shetani mkubwa wamezichoma moto bendera za Marekani na utawala khabithi wa Kizayuni. Nchi nyingine ambako kumeshuhudiwa maandamano makubwa zaidi ni Yemen, Lebanon, Syria, Iraq na Jordan.

Mamilioni nchini Iran

Nalo Taifa la Iran kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwa mara nyingine limebainisha wazi uungaji mkono wke kwa Quds Tukufu na watu wa Palestina sambamba na kutagaza kufungamana na Wapalestina katika mapambano ya Wapalestina dhidi ya madola ya kibeberu na kiistikbari duniani.Maandamano ya Kimataifa ya Siku ya Quds Kote Duniani Kuunga Mkono Palestina

Katika Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, sambamba na Siku ya Kimataifa ya Quds,  mamilioni ya wananchi wa Iran wamejitokeza kwa wingi katika Siku ya Kimataifa ya Quds kwa nara na kauli mbiu ya: "Siku ya Kimataifa ya Quds, Ushindi wa Mrengo wa Muqawama, Kushindwa Fitina ya Marekani na Wazayuni na Azam ya Taifa la Palestina Kurejea.

Waandamamanaji wametoa katika miji 900 mikubwa na midogo kote Iran wametoa  nara za "Mauti kwa Marekani", "Mauti kwa Israel", na "Mauti kwa Aal Saud na Wahaini Katika Eneo" hasa magaidi vibaraka na wakufurishaji vibaraka wa ISIS. Halikadhalika wananchi wa Iran wametangaa azma yao ya kuunga mkono ukombozi wa taifa la Palestina.

Washiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Iran walibeba pia mabango yenye kuulani utawala ghasibu wa Israel ambapo pia wametekteza mtoto bendera za utawala huo wa Kizyauni na vikaragosi vya rais Trump wa Marekani.

Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds aumefanyika katika miji mikubwa na midogo zaidi ya 900 kote Iran na kuhudhuriwa na wananchi pamoja na viongozi wa nazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ikumbukwe kuwa kufuatia ubunifu wa Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds. Katika siku hii Waislamu na wapenda haki kote duniani hujumuika ili kubainisha kuchukizwa kwao na sera za kibaguzi za utawala wa Kizayuni wa Israel huku wakitangaza kuunga mkono malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina.

/3466018

captcha