IQNA

Katika kutetea timu ya taifa iliyosoma Al Fatiha kabla ya mechi

Daktari Mpasuaji Tunisia asema husoma Qur'ani kabla ya kila Oparesheni

9:05 - June 23, 2018
Habari ID: 3471569
TEHRAN (IQNA)- Dhakir Lahidhab ni daktari mpasuaji ambaye Mtunisia ambaye katika kuwajibu wale waliokosoa hatua ya timu ya taifa ya soka ya nchi hiyo kusoma aya za Qur'ani kabla ya mechi na Uingereza katika Kombe la Dunia amesema binafsi husoma Qur'ani kabla ya kila oparesheni ya upasuaji.

Daktari Lahidhab ambaye ni mpasuaji wa moyo, amemjibu mmiliki wa vyombo vya  habari Mohammed Bugalab ambaye alipinga hatua ya kocha kuongoza wachezaji kusoma Surat al Fatiha kabla ya mechi ya Kombe la Dunia nchini Russia baina ya Tunisia na Uingereza Mnamo 18 Juni na kusema: "Hata kama suala hili linanihusu mimi binafasi, lakini Bugalab anapaswa kufahamu kuwa, kabla ya kila upasuaji mimi husoma Surat al Fatiha au aya nyiginezo za Qu'rani."

Ameendelea kuandika katika ukurasa wake wa Faceboo kuwa: "Baada ya kila upasuaji wa muda mrefu na wa masaa kadhaa, mimi husujudu kumshukuru Mwenyezi Mungu."

Daktari Lahidhab aidha anasisitiza Bugalab anataka kuidhalilisha dini ya Uislamu na amemtahadharisha kuwa dini si mchezo wa kisiasa.

Aidha Daktari Lahidhab anasema kabla ya hotuba yake katika kongamano muhimu la madkatari nchni Marekani, alisoma Surat al Fatiha.

Bugalab alimtuhumu vikali kocha wa timu ya taifa ya Tunisia Nabil Maaloul kwa hatua yake ya kuwaomba wachezaji kusoma Surat al Fatiha kabla ya mechi hiyo ambayo Uingireza iliibuka mshindi wa mabao mawili kwa moja. Alidai kuwa eti ucha-Mungi au taqwa si sharti la kushinda katika mechi. Lakini katika kujibu matamshi hayo hayo kocha Maaloul amesema: "Kila ambaye ananikosoa kwa kusoma al-Fatiha kabla ya mechi ya Uingereza na Tunisia anapaswa kupata matibabu. Sisi katika malezi yetu tumefunzwa al Fatiha na Qur'ani kwa ujumla tokea utotoni."

3724341

 

جراح تونسی: قبل از هر عمل قرآن می‌خوانم+عکس

جراح تونسی: قبل از هر عمل قرآن می‌خوانم+عکس

جراح تونسی: قبل از هر عمل قرآن می‌خوانم+عکس

جراح تونسی: قبل از هر عمل قرآن می‌خوانم+عکس

جراح تونسی: قبل از هر عمل قرآن می‌خوانم+عکس

جراح تونسی: قبل از هر عمل قرآن می‌خوانم+عکس

captcha