IQNA

Misikiti miwili yahujumiwa Brimingham, Uingereza

23:05 - August 17, 2018
Habari ID: 3471631
TEHRAN (IQNA)- Misikiti miwili imehujumiwa katika mji wa Birmingham nchini Uingereza katika tukio la chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Maafisa wa polisi waliofika katika eneo la tukio wanasema Jumatano wakati wa sala ya Ishaa, misikiti miwili ya Masjid Qamarul Islam na Masjid Al Hijrah ilihujumiwa katika mtaa wa Small Heath.
Polisi wanasema hujuma ya kwanza ilijiri saa nne usiku na ya pili dakika 20 baadaye ambapo madirisha ya misikiti hiyo yalivunjwa.
Msemaji wa Idara ya Polisi ya West Midlands amesema hujuma ya kwanza ililenga msikiti wa Qamarul Islam katika Barabra ya Foosbrooke saa nne usiku na ya pili ililenga msikiti wa Al Hijra katika Barabara ya Hob Moor dakika 20 baadaye.
Hayo yamejiri baada ya viongozi wa Msikiti Mkuu wa Birmingham kubainisha wasiwasi wao kuhusu kuongezeka vitendo vya hujuma za chuko dhidi ya Uislamu kufuatia tukio la Jumanne nje ya jengo la Bunge la Uingereza, katika mtaa wa Westminister mjini London siku ya Jumanne.
Katika tukio hilo la gari kugongan lango la Bunge la Uingereza, mshukiwa aliyekamatwa ni Muingereza Salih Khater ambaye ni mkazi wa Birmingham mwenye asili ya Sudan.

Khater ameshakamatwa na anakabiliwa na tuhuma za kutaka kuua na kutekeelza hujuma ya kigaidi. Kwa mujibu wa Nassar Mahmood, mmoja kati ya viongozi wa Msikiti Mkuu wa Birmingham, kumeshuhudiwa na ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu baada ya tukio hilo. Aidha amesema wanawake Waislamu wanaovaa Hijabu ndio ambao hukumbwa na masaibu zaidi kwa sababu mavazi yao yanafanya watambuliwe haraka .

3466543

captcha